IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia)

Ongezeko kubwa la  ualifu wa Chuki dhidi ya Uislamu, hujuma dhidi ya Misikiti nchini Ujerumani

21:32 - January 19, 2024
Habari ID: 3478217
IQNA - Tangu kuanza kwa vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 7, 2023, idadi ya jinai za chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu ikiwa ni pamoja na barua za vitisho zilizotumwa kwa misikiti nchini Ujerumani imeongezeka sana.

Hayo ni  kwa mujibu wa taarifa ya kitengo cha ubaguzi Taasisi ya Kituruki ya  Kiislamu na Masuala ya Kidini (DITIB) yenye makao yake makuu katika mji wa kaskazini wa Cologne. Taarifa hiyo imebaini kuwa barua nyingi na barua pepe zenye matusi na vitisho zimetumwa kwenye misikiti nchini Ujerumani.

Msikiti wa Kati wa Cologne pekee umepokea barua pepe na barua kwa njia ya posta 17, na hivi karibuni zaidi, Msikiti wa DITIB Selimiye katika mji wa kaskazini wa Dinslaken ulilengwa.

Kutokana na hali hii, Waislamu Ujerumani wanazidi kuwa na wasiwasi.

Mwezi uliopita, msikiti mmoja katika mji wa Munster magharibi mwa Ujerumani pia ulipokea barua ya vitisho iliyokuwa na matusi dhidi ya Waislamu na wahajiri.

Pia ilikuwa na matamshi ya kibaguzi, ikiwa ni pamoja na "Ujerumani kwa Wajerumani, wageni nje."

Mkuu wa Jumuiya ya Msikiti wa Munster Central, Fettah Cavus, alisema kuwa kwa masikitiko, chuki dhidi ya wageni na Waislamu inaongezeka nchini Ujerumani.

3486859

captcha